Tamasha na FinTech kuibua fursa za uwekezaji

DAR ES SALAAM: TAMASHA la Teknolojia ya Fedha FinTech linatarajiwa kuibua fursa mbalimbali na kuimarisha mifumo mbalimbali ya kiteknolojia nchini kwani linatarajiwa kuwakutanisha wawekezaji kutoka mataifa mbalimbali.

Akizungumzia wakati wa Ufunguzi wa tamasha hilo leo Alhamisi, jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Eastern Star Group, Deogratius Kilawe amesema tamasha hilo lina mawazo ya kuibua na teknolojia mpya iliyojaa midahalo na ushirikiano wenye tija na mitandao isiyo na kikomo ambayo inahusisha akili kubwa zaidi kutoka kwa ulimwengu wa fedha na teknolojia.

Ameongeza kuwa, tamasha la FINTECH lilianza mwaka 2016.

Advertisement

Katika katika tamasha lililopita, maazimio mbalimbali na tathmini na utekelezaji kwa mambo ambayo yalishidikana kipindi cha nyuma.

Amesema tamasha hilo litatoa fursa kwa wadau wote wa FINTECH kukutana kwa pamoja na kutathmini utekelezaji katika hatua zote ili kuweza kupiga hatua katika kufanikisha hilo.

“Mafanikio ya kuwezesha ujumuishwaji wa sekta ya fedha kuwa rahisi na kuwa mstari wa mbele wa kukuza Teknolojia ya FINTECH,” amesema.

Aidha, amesema tamasha hilo litawaleta pamoja Afrika Mashariki na kubadilishana ujuzi wa kimataifa kutoka kwa wasomi wakuu, watendaji na viongozi katika vipindi vilivyofikiriwa upya vinavyohusu kubuni, kujenga na kuhakikisha huduma endelevu za kifedha

Amesema tamasha la FINTECH ndilo tukio kubwa zaidi la Teknolojia ya Kifedha katika Afrika Mashariki, likitoa jukwaa kwa jumuiya ya FinTech kuungana, kushirikiana kwa pamoja.

1 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *