Tanesco wapongezwa usimamizi bora

WAKALA wa Nishati vijijini imeipongeza Shirika la Umeme nchini (TANESCO) Mkoa wa Mwanza kwa usimamizi mzuri na utekelezaji wa miradi sita ya umeme katika mkoa huo.

Pongezi hizo zimetolwa leo na Mwenyekiti wa Bodi ya Nishati vijijini (REA), Janet Mbene wakati mkutano wa siku moja na wakandarasi ,washauri wa miradi ya REA uliyofanyika leo mkoani Mwanza.

Mbene amesema kupitia mkutano huo wamejadili namna ya kuboresha miradi katika mikoa ya Kanda ya Ziwa kwa lengo la kufikia wananchi wote wapate umeme.

Amesema miradi sita ya umeme katika Mkoa wa Mwanza inayoendelea ni mradi wa REA III mzunguko wa kwanza,mradi wa REA III mzunguko wa pili,mradi wa ujazilizi awamu ya 2 A na mradi wa Peri Urban.

Ametaja miradi mingine ni mradi wa upelekaji umeme kwenye vituo vya afya na visima vya maji pamoja na mradi wa upelekaji umeme kwenye maeneo ya mgodi viwanda na kilimo.

Mbene amewataka wakandarasi kuhakikisha fedha za mradi zinatumika vizuri na miradi kukamilika kwa wakati.

“Mwisho wa mwaka huu kwa Mkoa wa Mwanza kila kijiji kitakuwa kimefikiwa na umeme. Baada ya vijiji tutaingia katika vitongoji. Nawapongeza wakandari wengi wapo katika hatua nzuri ya ukamilishaji wa miradi” amesema Mbene.

Kaimu Mkurugenzj wa Umeme vijijini (REA) Romanus Lwena amesema bodi yao imeridishwa na taarifa za miradi ya umeme inayotekelezwa katika Mkoa wa Mwanza.

Naye mhandisi wa miradi Shirika la Umeme(TANESCO) Mkoa wa Mwanza, James Kabasa ameishukuru REA kwa kuleta miradi ya umeme katika mkoa wa Mwanza.

Amesema mpaka sasa miradi mitatu imekamilika na mwezi Disemba mwaka huu miradi miwili itakamilika.

“REA imetusaidia sana kupunguza malalamiko kwa wananchi. Tunaiomba REA ituongeze pesa pamoja na miradi mingine ili tuweze kuwafikia wananchi wengi zaidi” amesema Kabasa.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
3 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Jobapplications
Jobapplications
3 months ago

Job applications

R (1).jpeg
Jobapplications
Jobapplications
3 months ago

Job application

OIP.jpeg
Tibirizi Chakechake Pemba
Tibirizi Chakechake Pemba
3 months ago

Usije dhani umejenga miji/Majiji Tanzania!? “TANZANIA YOTE NI VICHAKA TU HAKUNA NYUMBA HATA MOJA KAMA JANGWA LA SAHARA

Capture.JPG
Back to top button
3
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x