KATIKA kuhitimisha Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani, watumishi wanawake wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (TANGA UWASA), wametoa msaada wa mahitaji mbalimbali katika Hospitali ya Wilaya ya Pangani kama sehemu ya kurudisha kwa Jamii.
Akizungumza baada ya tukio hilo, Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo, Dk James Geotham Mrema ameshukuru kwa msaada huo muhimu kutoka kwa kuwakumbuka wagonjwa kupitia mahitaji mbalimbali na kuomba taasisi nyingine kuiga mfano huu
“Nawapongeza Wanawake wa TANGA UWASA kwa msaada wao katika maadhimisho haya ya Siku ya Wanawake Duniani, nitoe wito kwa taasisi na mashirika mengine kujitokeza na kuiga mfano huu. Sambamba na hilo nawatakia utekelezaji mwema wa majukumu yao”, amesema Dk James.
Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani kwa mwaka huu 2023, yamebebwa na kauli mbiu isemayo “Ubunifu na Mabadiliko ya Teknolojia chachu katika kuleta Usawa wa Kijinsia”.