KAGERA: Wakala wa Barabara (TANROAD) Mkoa wa Kagera umejipanga kukabiliana na athari za mvua kuhakikisha wanarejesha usalama wa barabara mkoani hapa kwa saa 24.
Meneja wa wakala huo mkoani hapa, Ntuli Mwaikosesya amesema kutokana na mvua kubwa iliyoanza kunyesha Machi mwaka huu timu ya wataalam wa uandishi kutoka ofisi yake wamejipanga kukabiliana na athari zote.
Amesema miongoni mwa barabara zilizoathirika hapo awali ni barabara ya Kasozibakaya _Kabindi_Nyantakara yenye kilometa 82 ambayo imeharibika Sshemu kidogo na madhara yake yamekabiliwa ndani yaasaa 24 na sasa inapitika vizuri na wananchi wanapata huduma.
“TANROAD tunahudumia mtandao wa Barabara zenye kilometa 2072 , na sasa Barabara zote zinapitika vizuri kwa sababu tuna vifaa,mitambo, waandisi na wakandarasi wako tayari kwa dharura yeyote ile ambayo itatokea wakati wa mvua , hii ni kuhakikisha wananchi hawakwami katika kupata huduma zote zinazohitajika ukizingatia kuwa tunaungana na nchi za Africa Mashariki hivyo tuko tayari kukabiliana na madhara ya mvua,” amesema Mwaikosesya
Amesema athari za mvua ya Elnino zilizosababisha madhara ya barabara na uhalibifu mkubwa kwa barabara maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Kagera tayari matengenezo yake yamekamilika kwa gharama ya Sh bilioni 4.6
“Barabara ya Nyabihanga -Minziro,mtukula _Bukoba,Bugene_Kaisho, Rutenge kishoju zimekamilika kwa asilimia 100 na wananchi wanaendelea kupata huduma kupitia Barabara hizo,”amesema
Ametoa wito kwa wananchi kuendelea kuchukua tahadhari pale wakiona maji yakikatiza kwa kasi katika barabara madaraja, kupungusha shughuli za kilimo karibu na kingo za Barabara, kuacha kuiba alama za barabarani , kuacha kutupa uchufu chini ya makatavati kwani hali hiyo imasababisha mitaro kuziba na kushindwa kupitisha maji .
TANROAD Mkoa wa Kagera imetenga bajeti ya Sh bilioni 12 kwa mwaka 2024/2025 kwa ajili ya matengenezo ya kawaida ya barabara hali inayopelelea kukabiliana na dharura wakati wowote.