TANROADS wabanwa, wataja wezi miundombinu ya barabara Tanga

TANGA: MKUU wa Mkoa wa Tanga, Waziri Kindamba amewataka Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) mkoani hapa kumsimamia mkandarasi anayejenga Daraja la Mto Pangani kuhakikisha linakamilika ifikapo mwaka 2025.

 

Akizungumzia katika kikao cha Bodi ya barabara amesema kuwa mkataba unaonesha daraja hilo lenye urefu wa mita 525 linatakiwa likamilike mwaka 2025 sambamba na kipande cha barabara cha chenye urefu wa kilometa 14.

Huku akiwataka TANROADS kumsimamia mkandarasi anayejenga Barabara ya Tanga-Pangani kukamilika kwa kiwango cha lami ifikapo mwezi Machi, 2024.

 

“Tunachotaka hii barabara na daraja viweze kukamilika kwa wakati Ili kufungua uchumi wa wilaya ya Pangani lakini na mkoa kwa ujumla,” amesema RC Kindamba.

Naye Kaimu Meneja wa TANROADS Mkoa wa Tanga, Mhandisi Zuhura Aman amesema kuwa kumekuwa na changamoto ya wizi na uharibifu wa miundombinu ya barabara ikiwemo alama za barabarani.

 

Amesema kuwa wizi huo wa miundombinu umekuwa ukiisababishia hasara Serikali kwa kuweka alama hizo mara kwa mara huku wananchi wakiziiba kama vyuma chakavu.

Habari Zifananazo

Back to top button