Tantrade waandaa shindano nembo ya taifa

DAR ES SALAAM :Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania ( TANTRADE) imeandaa shindano la kutengeneza logo ya Made In Tanzania itakayotumika kama nembo ya bidhaa na huduma zinazotengenezwa nchini Tanzania.

Logo hiyo ambayo ni sehemu ya mpango wa nembo ya taifa inalenga kuwa ishara ya taifa inayounganisha na kuwakilisha ubora na upekee wa bidhaa na huduma za Tanzania katika soko la kitaifa na kimataifa.

Akitangaza shindano hilo leo jijini Dar es salaam kwenye mkutano na waandishi wa habari Mkurugenzi Mkuu wa TanTrade, Latifa Khamis amesema lengo la shindano hilo ni kuhakikisha bidhaa za Tanzania zinafahamika zaidi ili kuimarisha ushindani wa bidhaa na huduma za Tanzania na kuvutia wawekezaji  huku ikiakisi nguvu ya viwanda na vipaji vilivyopo nchini .

Akitaja zawadi zitakazotolewa amesema mshindi wa kwanza atazawadiwa zawadi ya Sh milioni 3 mshindi wa pili Sh milioni 2 na watatu atapata Sh milioni 1.

Shindano hilo linahusisha wabunifu wa picha na wasanii kutoka katika mikoa yote nchini huku ikilenga pia kumjengea mshindi historia ya kuacha alama kwa taifa.

Habari Zifananazo

Back to top button