TanTrade yatunukiwa cheti cha CCAA

MAMLAKA ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) imepokea cheti cha Chaguo la Mteja Afrika (CCAA).

Hafla hiyo ya utoaji tuzo  kwa Kampuni mbalimbali zinazotoa huduma kwa wananchi imefanyika jijini Dar es Salaam.

TanTrade imepokea cheti hicho kwa kuitambua kama mlezi wa tuzo hizo na kushiriki katika kuiwezesha kufanyika tangu zilipoanzishwa mwaka 2019 hapa nchini.

Mkurugenzi Mkuu wa TanTrade Latifa Khamis, amekabidhiwa cheti hicho  na Naibu Waziri wa Uwekezaji ,Viwanda na Biashara Exaud Kigahe (Mb) ambaye alikuwa mgeni rasmi.

Tuzo hizo zilihudhuriwa pia na Msanii maarufu wa filamu kutoka nchini Naigeria Iniobong Edo  zimefanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.

Habari Zifananazo

Back to top button