Tanzania, Canada zaimarisha mafunzo ujuzi kwa wanawake, wasichana

TANZANIA kwa kushirikiana na Jumuiya ya Vyuo na Taasisi za Ufundi Canada (CiCan) inatekeleza Mradi wa Uwezeshaji kupitia Ujuzi (ESP) unaolenga kuongeza ushiriki wa wanawake na wasichana katika shughuli za kiuchumi na kijamii.
Mradi huu ni sehemu ya jitihada za Serikali ya Tanzania kuboresha elimu ya ufundi stadi na kutoa fursa kwa makundi yaliyo katika mazingira hatarishi, hususan wanawake na vijana wa vijijini.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dk Wilson Mahera,
Akizungumza katika Mkutano wa kutathmini ya utekelezaji wa Mradi huo jijini Arusha, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dk Wilson Mahera, ameeleza kuwa mradi huo umekuwa na matokeo chanya, hasa kwa mabinti waliotoka katika mazingira magumu na waliokuwa wameacha shule.
Amesema kupitia Vyuo vya Maendeleo ya Wananchi, walengwa wamepata mafunzo ya ushonaji, mapishi, na stadi nyingine za maisha zitakazowawezesha kujitegemea.
Mkurugenzi wa Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi, kutoka Wizara hiyo Dk Fredrick Salukele, amesema vyuo 54 vya FDCs vimehusika moja kwa moja katika mradi huo, huku vyuo 12 vikishirikiana na vyuo kutoka Canada ili kubadilishana maarifa na kuongeza ufanisi wa programu.
Kwa upande wake, Mkuu wa Ushirikiano katika Ubalozi wa Canada nchini Tanzania, Carol Mundle, amesisitiza dhamira ya Canada katika kusaidia vijana na wanawake kupitia miradi ya mafunzo ya kiufundi na ujasiriamali, akisisitiza kuwa mpango huu unaendana na vipaumbele vya usawa wa kijinsia na maendeleo jumuishi.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button