Tanzania kupambana mabadiliko tabia nchi

SERIKALI imesaini mkataba wa makubaliano ya ushirikiano na Shirika la NORAD la nchini Norway kwa ajili ya tafiti za kupambana na mabadiliko ya tabia nchi, kwa ufadhili unaogharimu Sh bilioni 9.

Makubaliano hayo yamefikiwa Dar es Salaam na Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) Dk Amos Nungu pamoja na Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Watu kutoka Balozi za Norway na Sweden Lisa Sivertsen, na kushuhudiwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Dk Selemani Jafo akiwa na Balozi wa Norway nchini Tonne Tines na Balozi wa Sweden Charlotta.

Akizungumza Jafo amesema makubaliano hayo yamefikiwa baada ya mkataba uliosainiwa Septemba mwaka huu wa ushirikiano na Norway wa program ya miaka mitano ya kupambana na mabadiliko ya tabia nchi inayotekelezwa na Costech.

Advertisement

Amesema fedha hizo zilizotolewa na Norway zitatumika na watafiti nchini kwa ajili ya mabadiliko ya tabia nchi kwa kuangalia namna ya kupunguza athari.

” Athari za mabadiliko ya tabia nchi ni wazi zinaonekana ikiwamo barafu kuyeyuka, uharibifu wa miundombinu na hata ukame,” amesema na kuongeza kuwa ajenda ya tafiti nchini itakuwa kubwa sana na kwamba Sweden imekubali kushirikiana pia.

Amewaomba watafiti kujikita kufanya tafiti zenye kuleta tija Kwa matatizo yanayoikumba jamii kwamba kama ni eneo la kilimo hali iweje na pia miundombinu ujenzi wake uwe wa namna gani.

Kwa upande wake Nungu amesema fedha zilizotolewa na Norway zimepitia chini ya mfumo wa Sayansi na Teknolojia ili kufadhili tafiti katika eneo hilo.

Amesema kupitia programu hiyo watafiti watoe mapendekezo yao Ili kutafuta changamoto za tabia nchi.

Balozi wa Norway Tinnes amesema ufadhili huo ni sehemu ya makubaliano yaliyofikiwa Kwa ajili ya kukubaliana na kupunguza suala zima la mabadiliko ya tabia nchi.

Amesema mradi huo unahusisha tafiti zinazoweza kutoa elimu kuhusu tabia nchi ambazo zitawasiaida watanzania kuweza kujua kwa kina kuhusu mabadiliko ya tabia nchi athari na namna ya kukabiliana nayo.

Balozi wa Sweden, Macias amesema mradi utaongeza uwezo wa watanzania katika tafiti na kuimarisha taasisi kuhusu tabia nchi na kwamba wako tayari kushiriki.

4 comments

Comments are closed.