Tanzania, Msumbiji kudumisha diplomasia

MABALOZI wa Serikali ya Tanzania na Msumbiji wamefanya kikao cha ujirani mwema juu ya kudumisha uhusiano wa kiuchumi kwa nchi hizo mbili.

Akizungumza mkoani Mtwara, Balozi wa Tanzania nchini Msumbiji Phaustine Kasike amesema licha ya nchi hizo kuwa na ushirikiano mkubwa wa kihistoria hasa kwenye upande wa siasa na kijamii.

“Hali imekuwa tofauti kwa upande wa kiuchumi kwani bado haujafikia kiwango cha kulidhisha hivyo kupitia mikutano ya ujirani mwema itakuwa fursa ya kuwezesha nchi ya Tanzania kutangaza fursa zake za uchumi zilizopo kwenye maeneo ya kilimo, viwanda, utalii na biashara zitazosaidia kupata masoko,”amesema Kasike

Kikao hicho kimefanyika katika manispaa ya Mtwara Mikindani lengo likiwa ni pamoja na kuimarisha vikao vya ujirani mwema kwa nchi hizo mbili na kudumisha uhusiano pamoja na kukuza uchumi kwa mkoa na wananchi kwa ujumla.

Naye Balozi wa Msumbiji nchini Tanzania Ricardo Ambroisio amesema manufaa ya kikao hicho ni kuona namna ya majimbo mawili kati ya Cabo Delgado na Mtwara yanaweza kunufaika nayo.

Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Kanali Patrick Sawala ameyaomba mataifa hayo mawili kupitia mabalozi wake kuendeleza ujirani mwema katika nyanja mbalimbali ambapo nyanja ya kiuchumi kiwe kipaumbele.

Aidha ameweka wazi hatua ya mataifa hayo mawili ambayo tayari jitihada za kuunganisha mawasiliano baina ya watu wake zimeanza kuchukuliwa katika mipaka yake na tayari wamesharekebisha kivuko cha MV Kilambo.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button