Tanzania mwenyeji G25 wazalishaji Kahawa

TANZANIA  imepitishwa kuwa Mwenyeji wa mkutano mkubwa wa Nchi 25 wazalishaji wa zao la Kahawa Afrika(G-25).

Hayo yamesemwa katika Mkutano wa pili wa nchi wazalishaji wa zao la Kahawa Afrika uliofanyika Jijini Kampala,Uganda na kufunguliwa na Rais wa Jamhuri ya Uganda Yoweri Kaguta Museveni.

Katika Azimio la Kampala (Kampala Declaration) imetamka bayana kwamba Mkutano wa tatu wa nchi wazalishaji wa Kahawa Afrika utafanyika Tanzania mwaka 2024 na hivyo azimio hilo kuitangaza Tanzania kama Mwenyeji wa mkutano huo mkubwa wa Kahawa Afrika.

Akizungumza katika Mkutano huo,Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango ameeleza bayana mikakati ya kukuza zao la kahawa nchini.

Amesema Tanzania imeongeza  bajeti ya Wizara ya kilimo ambapo juhudi nyingi zimeelekezwa katika utafiti na uzalishaji wa miche bora ambayo husambazwa kwa wakulima kwa lengo la kuongeza uzalishaji wa zao la kahawa ambapo uzalishaji wa zao hilo umeongezeka kutoka Tani 66,543 mwaka 2021/22 hadi kufikia Tani 82,491 kwa mwaka 2022/2023.

Aidha Dkt. Mpango alitumia fursa hiyo kuwaalika nchi wazalishaji wa zao la kahawa katika mkutano wa tatu wa nchi 25 (3rd G-25 Africa Coffee Summit 2024) wazalishaji wa Kahawa Afrika utakaofanyika nchini Tanzania mwaka 2024.

Katika Ujumbe wake Makamu wa Rais ameongozana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mh. Balozi Mbarouk N. Mbarouk,Naibu Waziri wa Kilimo Mh. Anthony P. Mavunde na wataalamu kutoka Bodi ya Kahawa Tanzania.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
5 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
NBC_corporateservices@nbctz.com
NBC_corporateservices@nbctz.com
1 month ago

NBC RAIS WA TANZANIA NI NYERERE

MAPINDUZI HALISI YA WAPAMBANAJI.PNG
NBC_corporateservices@nbctz.com
NBC_corporateservices@nbctz.com
1 month ago

NBC RAIS WA TANZANIA HADI SASA NI NYERERE

MAPINDUZI HALISI.PNG
NBC_corporateservices@nbctz.com
NBC_corporateservices@nbctz.com
1 month ago

RAIS WA TANZANIA HADI SASA NI NYERERE

MAPINDUZI.jpg
NBC_corporateservices@nbctz.com
NBC_corporateservices@nbctz.com
1 month ago

RAIS WA TANZANIA HADI LEO NI NYERERE

MAPINDUZIII.PNG
NBC_corporateservices@nbctz.com
NBC_corporateservices@nbctz.com
1 month ago

RAIS WA TANZANIA HADI WAKATI HUU NI NYERERE

MAPINDUZIIII.PNG
Back to top button
5
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x