Tanzania, Vietnam kuongeza ushirikiano wa kiuchumi

VIETNAM: JAMHURI ya Muungano wa Tanzania na Jamhuri ya Kijamaa ya Vietnam zimeafikiana kuongeza maeneo mapya ya ushirikiano wa kiuchumi na kijamii, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kukuza maendeleo kwa mataifa yote mawili.

Makubaliano hayo yamefikiwa katika mazungumzo yaliyofanyika jijini Hanoi kati ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mahmoud Thabit Kombo , na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Vietnam, Bui Thanh Son.

Maeneo mapya ya ushirikiano yaliyopewa kipaumbele ni pamoja na uanzishwaji wa viwanda vya kuongeza thamani kwenye mazao ya kilimo kama korosho, matunda, na mbogamboga, pamoja na teknolojia.

SOMA:Waziri Kombo awasili Vietnam

 

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button