Tanzania wachanguliwa mpango wa kimkakati

Tanzania imechaguliwa kuwa moja ya nchi nane za Afrika zitakazopewa kipaumbele na Italia kupitia mpango mpya wa kimkakati wa Mattei (Mattei Plan).

Akizungumza leo, Januari 29, 2024 Rais wa Chama cha Wafanyabiashara wa Italia, Mhandisi Alfredo Cestari amesema kiasi cha Euro bilioni 5 za awali zimetengwa kwa ajili ya utekelezaji wa miradi hiyo.

Mhandisi Cestari amesema hayo alipokutana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, January Makamba pembezoni mwa Mkutano wa Nne wa Wakuu wa Nchi za Afrika na Italia unaendelea Roma, Italia.

Advertisement

Aidha, Mhandisi huyo alieleza kuwa utekelezaji wa mpango huo utaanza mara baada ya kumalizika kwa mkutano wa Wakuu wa nchi za Afrika na Italia, ambapo Serikali ya nchi hiyo itafadhili miradi ya kipaumbele kwa nchi nane za awali za Afrika.

“Hatua hiyo itahusisha pia kugharamia gharama za upembuzi yakinifu ya miradi itakayopendekezwa,” alisema Mhandisi Cestari

Kama hatua ya utekelezaji ya mpango huo, ujumbe wa wataalam kutoka Chemba ya Biashara ya Italia ikiongozwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Italia, Dk  Edmondo Cirielli unatarajiwa kuwasili Tanzania kwa ajili ya kukutana na timu ya wataalam ya upande wa Tanzania kwa ajili ya kukamilisha hatua za awali za utiaji saini wa ushirikiano huo wa pande mbili utakaohusisha utekelezaji wa miradi itakayopitishwa na pande mbili.

Pamoja na mambo mengine, mkutano huo umelenga kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji ili kuongeza kiwango cha biashara na uwekezaji baina ya Tanzania na Italia kupitia mpango mpya wa Mattei (Mattei Plan).

Miradi hiyo ya kipaumbele kupitia Mpango mpya wa Kimkakati wa Mattei (Mattei plan) ipo katika sekta ya nishati, elimu na kilimo. Ethiopia,

/* */