Tanzania yajipanga kwa COP11 Geneva

UJUMBE wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania umefika mjini Geneva tayari kuanza Mkutano wa 11 wa Nchi wanachama wa Mkataba wa WHO wa Kudhibiti Tumbaku (WHO FCTC COP11 ), unaofanyika Geneva , Uswiss tarehe 17–22 Novemba 2025.
Ujumbe huu unaongozwa na Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania Umoja wa Mataifa, Balozi Abdallah Saleh Possi, na unajumuisha wataalam kutoka Wizara ya Afya, Fedha, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kilimo, Uwekezaji, Viwanda na Biashara.
Katika picha ni aliyekuwa Balozi wa Tanzania Geneva na Italia Dk. James Msekela ambaye ni miongoni mwa ujumbe huu. Kushoto ni Mwakilishi wa Kudumu Geneva Balozi Dk. Abdallah Possi na kulia ni Naibu Mwakilishi wa Kudumu Balozi Dk. Hoyce Temu.
Tanzania inaendelea kuonyesha dhamira ya kulinda afya ya umma na kuimarisha mikakati thabiti ya kudhibiti matumizi ya tumbaku kimataifa. SOMA: TMDA ‘yakomaa’ viwango WHO



