TIMU ya Tanzania ya olimpiki ya mpira wa wavu kwa wanawake, imeanza vyema kampeni yake katika michuano ya Olimpiki maalumu kwa kuibuka na ushindi wa pointi 25-10 dhidi ya Italia, katika mchezo wa awali wa kufuzu hatua ya pili ya mchujo kwenye michuano hiyo inayoendelea nchini Ujerumani.
Michuano hiyo maalumu inafanyika katika mji wa Berlin nchini Ujerumani, ambapo mataifa mbalimbali yanashiriki michuano hiyo, Waziri wa Sanaa utamaduni na Michezo Dk Pindi Chana, alikuwa shuhuda wakati bendera ya Tanzania ikipepea nchini Ujerumani.
Mwanariadha Mathias Makanyaga kutoka Tanzania, ameshika nafasi ya tatu kwenye mbio za meta 800 na hivyo kufuzu fainali, ambapo kesho atatupa karata yake fainali.
Katika mchezo mwingine timu ya wanaume ya mpira wa wavu imepoteza dhidi ya Botswana, lakini timu hiyo imesonga mbele katika hatua inayofuata.