Tanzania yashiriki mkutano Baraza la Haki za Binadamu Uswisi

Tanzania yashiriki mkutano Baraza la Haki za Binadamu Uswisi

MKUTANO wa 51 wa Baraza la Haki za Binadamu unaendelea Geneva, Uswisi, huku ujumbe kutoka Tanzania unaongozwa na Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Prof. Eliamani Sedoyeka.

Mkutano huo ulianza jana Jumatatu na unatarajiwa kumalizika Oktoba 7, mwaka huu.

Taarifa iliyotumwa kwenye vyombo vya habari, inasema kuwa miongoni mwa ajenda ambazo Tanzania imejipanga kuzungumzia ni pamoja na haki ya maendeleo kwenye elimu, afya, makazi, maji salama na usafi.

Advertisement

Pia mkutano huo  utazungumzia athari za Uviko 19, hasa katika sekta  na mikakati madhubuti iliyowekwa ya kudhibiti uchumi dhidi ya janga hilo, ikiwemo kuhimiza  utoaji wa chanjo ya uviko na kutangaza nchi kupitia Royal Tour.

/* */