NIGERIA: TIMU ya taifa ya wanawake chini ya miaka 20 ‘Tanzanite Queens’ inaingia dimbani leo kuvaana na Nigeria katika Uwanja wa Moshood Abiolo, jijini Abuja.
–
Katika mchezo huo wa kuwania kufuzu Kombe la Dunia nchini Colombia mwaka 2024, Quuens inawalazimu kupata matokeo chanya ya ushindi au kutoka sare ya 2-2, kufuatia mchezo wa awali wa Novemba 12, 2023 kutoka sare ya 1-1 katika Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam.
–
Kocha Mkuu wa Tanzanite Queens, Bakari Shime amesema wanauendea mchezo huo kwa mbinu tofauti na ya awali lakini ana imani na wachezaji wake kwakuwa wana uzoefu wa kutosha kukabiliana na michezo migumu na ya kishindani.
–
Akizungumzia juu ya utayari wa wachezaji wenzie, Nahodha wa timu hiyo Noela Luhala amesema kama wachezaji wamejiandaa vyema kuwakabili wapinzani wao
–
“Tumewafahamu vizuri wapinzani wetu kupitia mchezo wetu wakwanza, na tumefahamu wapi walikuwa na mapungufu na wapi nasi tulikosea. Tuliyoelekezwa na Mwalimu wetu katika uwanja wa mazoezi naamini tunaenda kuyatekeleza.” Amesema Luhana.
–
Imeandaliwa na @ismailykawambwa
–
Una maoni usisite kutuandikia
–
Je umejisajili #MwangwiwaUkarimu #EchoesofKindness #MwangwiwaUkarimu #ukarimu #mabingwa #Jarida #mwangwiwahadithi #Mashujaa #shujaawangu
#HabarileoUPDATES