Taswa waipongeza Stars

CHAMA cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA) kimelipongeza Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Kaimu Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Hemed Suleiman ‘Morocco’, wasaidizi wake na wachezaji wa Taifa Stars kwa kufuzu fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) zitakazofanyika mwaka 2025 nchini Morocco.

Taarifa iliyotolewa leo Novemba 20, 2024 na chama hicho imewapongeza pia wananchi waliofika uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam, kuiunga mkono Taifa Stars.

“Tunawasihi Watanzania tuendelee kuiunga mkono Taifa Stars, kwani safari bado ni ngumu na ndefu. Ni vizuri kwa mshikamano ambao tumeonesha hadi tukafanikiwa kuvuka kizingiti na kupata tiketi ya kwenda Morocco tukauendeleza kwa kasi zaidi,”

Advertisement

“Tunaomba matayarisho kwa fainali za mwakani yaanze mara moja na kila mwenye uwezo ajitokeze kuisaidia Taifa Stars, kwani ushindi wao ni wa kulijengea heshima taifa letu,” imeeleza taarifa hiyo.