Tathmini ya ukusanyaji kodi wa TRA 1996 – 2022

UCHANGANUZI wa takwimu za kodi unatoa uelewa kuhusu mifumo na tofauti za mapato ya kodi.

Takwimu hizo zinajumuisha kodi za bidhaa mbalimbali na mapato yake kuanzia mwaka 1996/1997 hadi 2023/2024. Zi[1]naonesha pia idadi ya bidhaa za kodi zilizorekodiwa kila mwaka pamoja na mabadiliko katika ukusanyaji wa takwimu.

Hii inamaanisha kuwa si bidhaa zote za kodi zilikuwa na takwimu kamili kila mwaka. Kimsingi, kumekuwa na ongezeko la ukusanyaji wa mapato mwaka hadi mwaka ukionesha ukuaji katika utendaji wa jumla wa kodi.

Advertisement

Kimsingi, takwimu za mapato ziliongezeka sana katika miaka ya baadaye, zikionesha mifumo bora ya ukusanyaji kodi au ukuaji wa uchumi. Katika kipindi cha 1996/1997 hadi 2000/2001, wastani wa mapato ya kodi ulikuwa chini ikilinganishwa na miaka iliyofuatia baadaye.

Tofauti na hapo, mapato katika miaka ya 2018/2019 hadi 2023/2024 yamepanda kwa kasi na kufikia mamilioni kwa wastani wa makusanyo. Hii inaashiria kuwapo ufanisi katika ukusanyaji kodi au mabadiliko katika shughuli za kiuchumi kama vile ongezeko la pato la viwanda au vyanzo vya kodi.

Kipindi cha kutoka mapato ya chini hadi ya juu zaidi kinaonesha kuimarika kwa mfumo wa kodi kadri miaka inavyoendelea.

Takwimu zinaonesha pia tofauti katika michango ya bidhaa za kodi kila mwaka. Wakati baadhi ya bidhaa za kodi zikichangia kwa kiasi kikubwa, nyingine huwa na mapato ya chini au zaidi yanay[1]opanda na kushuka yakiashiria viwango tofauti vya utegemezi katika vyanzo mbalimbali vya kodi.

Aidha, mwenendo imara wa kupanda katika ukusanyaji kwa wastani unalingana na mifumo ya ukuaji wa uchumi. Hii inaashiria kuwa, yapo mambo kadhaa yakiwamo ya ukuaji wa viwanda, mabadiliko ya sera au kuboreshwa kwa uwezo wa kiutawala yaliyochangia kuimarika ukusanyaji wa mapato ya kodi.

Hali hii inadhihirishwa kwa kuzingatia mambo yanayochochea ukuaji wa uchumi yakiwa[1]mo ya uzalishaji na ukuaji wa mapato ili kuendeleza ukuaji huo. Uchambuzi wa mwenendo Kubainika kwa ongezeko la makusanyo ya kodi kunatoa uelewa muhimu wa mwenendo wa kiuchumi na kifedha wa Tanzania Bara tangu mwaka 1996 hadi 2022.

Kodi zinazohusiana na mapato ikiwamo Kodi ya Mshahara (PAYE), kodi za mashirika, kodi za watu binafsi na nyinginezo, huthibitisha ukuaji imara huku PAYE ikibainika kuwa kodi inayofanya vizuri zaidi. Ukuaji huu unaashiria ongezeko la ajira rasmi na kupanda kwa mishahara, sambamba na ubora katika kutekeleza masuala ya kodi.

Ingawa kodi ya mashirika inaonesha mwelekeo wa juu zaidi, kupanda na kushuka kwake kunaashiria utulivu wenye tija katika mzunguko wa kiuchumi na mabadiliko ya sera. Ongezeko la kodi kwa watu binafsi linaelekea katika ongezeko la wigo wa walipa kodi, au mifumo iliyoboreshwa ya kukusanya na kuripoti.

Hata hivyo, tofauti ka[1]tika kodi nyingine za mapato inaashiria hali isiyotabirika ya mapato. Kodi za ndani na zinazo[1]husiana na uagizaji bidhaa pia zinaonesha ukuaji mkubwa na nafasi muhimu katika mfumo wa kodi. Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) na ushuru wa bidhaa linaonesha ongezeko kubwa linalochochewa na ku[1]panda kwa matumizi ya ndani na usimamizi bora wa kodi.

Aidha, VAT katika kuagiza bidhaa na ushuru wa bidhaa huonesha mwelekeo bora unaoakisi ongezeko la biashara na utozaji bora wa ushuru wa uagizaji bidhaa. Kati ya hizi, VAT katika kuagiza na kuuza bidhaa ndani na nje ya nchi, ni nguzo imara katika muundo wa kodi ikionesha matumizi makubwa katika wigo mpana wa huduma na bidhaa mbalimbali.

Hata hivyo, makundi kama vile ada nyingine za uagizaji bidhaa na kodi nyingine za ndani zinatofautiana kidogo katika uzalishaji wa mapato.

Uchambuzi wa wachangiaji kodi Uchambuzi kuhusu wachangiaji wakuu wa kodi kwa miaka mingi unaonesha mabadiliko ya vyanzo vya mapato ya kodi nchini Tanzania.

Mara nyingi PAYE ni mchangiaji mkubwa ikiakisi kukua kwa sekta rasmi ya ajira na ukusanyaji wa kodi unaotegemewa kutoka kwa watu wanaolipwa mshahara. Kodi ya mashirika pia ina nafasi kubwa ingawa michango yake inaonesha kushuka kwa thamani kunakoweza kuathiriwa na faida za kampuni, mzunguko wa kiuchumi na mabadiliko ya sera ya kodi.

Kwa pamoja, kodi hizi za mapato ni muhimu kwa ukuaji wa uchumi. Kodi zinazotokana na matumizi hasa VAT ya ndani na VAT katika uagizaji zimeonesha ukuaji mkubwa siku hadi siku na hivyo kuonesha umuhimu wake katika mfumo wa kodi. Ongezeko thabiti la VAT ya ndani linaonesha ongezeko la matumizi ya ndani na utekelezaji bora wa VAT, huku  VAT katika uagizaji bidhaa ikitegemea zaidi biashara ya kimataifa kama kichocheo cha mapato.

Makundi yote mawili yanaonesha umuhimu wa kodi ya matumizi kutokana na shughuli za kiuchumi. Ingawa kodi ya uagi[1]zaji ni thabiti, pia ni mchangiaji muhimu ikiakisi kiasi cha biashara thabiti na muundo wa kodi uliowekwa.

Mwelekeo huu kwa pamoja unasisitiza haja ya kuwa na sera zinazowiana ili kukabilia na kuimarisha michango mbalimbali na inayobadilika ya mapato, matumizi na kodi zinazoegemea biashara katika mapato ya taifa.

Uchanganuzi unasisitiza haja ya mbinu za kisera zenye uwiano ili kudumisha na kuimarisha vyanzo hivi vya mapato, kuhakikisha kuna uthabiti dhidi ya kushuka kwa uchumi. Uchambuzi wa marejesho ya kodi Mwenendo wa marejesho ya kodi tangu mwaka 1996 hadi 2022 unaonesha ongezeko thabiti la marejesho ya kodi na unyeti wa miamala ya kodi kwa uchumi unaopanuka.

Mwelekeo huu unahusishwa na makusanyo ya juu zaidi ya kodi, kwa kuwa malipo ya ziada yanahitaji marekebisho. Ongezeko hilo linaashiria uboreshaji katika usimamizi ili kuruhusu mamlaka ya kodi kushughulikia marejesho kwa ufanisi zaidi.

Katika kutathimini urejeshaji wa kodi kama ukuaji wa mapato kwa asilimia, takwimu zinaonesha mwelekeo mzuri na ongezeko la mara kwa mara. Ongezeko la mara kwa mara katika viwango vya urejeshaji fedha huenda likalingana na mabadiliko ya sera, kama vile kuanzishwa kwa vivutio vipya vya kodi, punguzo au marekebisho yanayotokana na ukaguzi na utekelezaji wa sheria.

Mabadiliko ya kodi Mabadiliko ya kodi huzingatia mwitikio tofauti wa mapato ya kodi kwa viashiria muhimu vya kiuchumi. Mapato ya kodi yanaonesha mabadiliko ya chini, lakini thabiti kwa Pato la Taifa la Jumla (GNI) na yanakua taratibu kuliko mapato na kuashiria picha ndogo ya ukuaji wa mapato. Mabadiliko katika pato la uzalishaji hubadilika sana ya[1]kionesha michango isiyowiana ya viwanda inayoendeshwa na mabadiliko ya sera au ya kiuchumi. Mapato huitikia taratibu uagizaji na kuashiria umuhimu wa kodi za biashara ingawa uboreshaji katika ufanisi unaweza kuongeza mwitikio wa ajira.

Tofauti ya mwitikio wa mabadiliko kutokana na GNI na idadi ya watu, huonesha vipa[1]umbele vya kimuundo ndani ya mfumo wa kodi.

Mapato ya kodi huonesha mabadiliko ya hali ya juu kutegemeana na idadi ya watu na hukua kwa kasi zaidi kuliko idadi ya watu na hivyo, kuhitaji kuboreshwa kwa ukusanyaji wa kila mtu na kupanua wigo wa kodi.

Mwenendo huu unasisitiza mwendelezo katika uboreshaji wa mfumo wa kodi kwa kuwa kodi zisizo za moja kwa moja kama vile VAT, kodi za matumizi na kodi za biashara hukamata shughuli za kiuchumi zinazoendeshwa na idadi ya watu kwa ufanisi zaidi.

Ongezeko la idadi ya watu mara nyingi huongeza wigo wa kodi kwa kuongeza matumizi na kuwezesha utekelezaji bora wa usimamizi hasa katika ukuaji wa miji na ukuaji rasmi Wakati matumizi yanayotokana na idadi ya watu yakiongeza mapato ya kodi, mwitikio mdogo kutokana na GNI unaonesha kutofaulu katika ukusanyaji wa kodi ya mapato.

Hii inatokea kutokana na kutegemea kodi zisizo za moja kwa moja, utekelezaji duni katika sekta zisizo rasmi, na kutotozwa kodi za kutosha kwa makundi. Kushughulikia mapengo haya, hasa katika mwitikio wa kodi ya mapato na viwanda, kunaweza kukamilisha utendaji thabiti unaohusishwa na ongezeko la watu na kuimari[1]sha ufanisi wa jumla wa mfumo wa kodi.

Hitimisho Mabadiliko ya mfumo wa kodi nchini Tanzania yanaonesha kuwapo maendeleo makubwa katika ukusanyaji wa mapato na kushughulikia changamoto kadhaa zinazohusu ufanisi mdogo kimuundo, kutofautiana kwa michango na upungufu katika mifumo ya utawala na sera. Tofauti katika michango ya kodi hasa kutoka kwa makundi kama vile kodi za mashirika na kodi nyingine za mapato, husababisha changamoto za upangaji wa fedha kutokana na unyeti kwa mizunguko ya kiuchumi na mabadiliko ya sera.

Kimsingi, upungufu wa kimuundo kama vile mwitikio mdogo kwa Pato la Taifa la Jumla (GNI), unaonesha ufanisi mdogo katika ukusanyaji wa kodi ya mapato unaotokana na msingi finyu wa kodi, utekelez[1]aji hafifu na utegemezi wa kodi zisizo za moja kwa moja.

Mapato yatokanayo na uzalishaji wa viwanda na kodi za mashirika pia yanashuhudia michango isiyo sawa inayoweza kuchochewa na sera mahususi za sekta na kushuka kwa uchumi, wakati mwitikio wa wastani kwa ushuru wa biashara unaonyesha kutofaulu katika kutumia biashara ya kimataifa kwa ukuaji wa mapato.

Kuongezeka kwa urejeshaji wa kodi, ingawa kunaweza kuashiria ufanisi wa usimamizi, kunaakisi changamoto katika tathmini sahihi za kodi na matatizo yanayosababishwa na malipo ya ziada kwenye mapato halisi.

Kwa nyongeza, unyumbufu mkubwa wa ukuaji wa idadi ya watu unaonesha maendeleo katika ufanisi wa ukusanyaji wa kodi, lakini ukuaji wa haraka wa miji na shughuli za kiuchumi zisizo rasmi huleta hatari za upungufu katika usimamizi.

Ongezeko la mara kwa mara na kushuka kwa aina fulani kwa kodi zikiwamo kodi nyingine za ndani na kodi za uagizaji, linaonesha kutowiana katika usimamizi na utekelezaji wa sera, na hivyo kudhoofisha uthabiti wa fedha. Kunahitajika ushirikishwaji wa pamoja ili kukabiliana na changamoto hizi na kutafuta suluhu za kiutendaji.

Jambo hili litaiwezesha Tume ya Rais ya Maboresho ya Kodi kuwa uwezo wa kuandaa mapendekezo yanayotekeleze[1]ka ya namna ya kuanzisha mfumo thabiti na himilivu wa kodi kwa mustakabali wa Tanzania. Jukumu hili muhimu ndilo tunalolenga kufanya kuanzia wiki ijayo.