TCB yajivunia mafanikio mradi wa SGR
Deprecated: htmlspecialchars(): Passing null to parameter #1 ($string) of type string is deprecated in /home/habarileoacc/public_html/wp-includes/formatting.php on line 4720
DAR ES SALAAM: Benki ya Biashara Tanzania (TCB) imesema inajivunia kuwa sehemu ya mradi wa reli ya kisasa (SGR) uliozinduliwa hivi karibuni kwa safari ya kutoka Dar es Salaam kwenda Dodoma.
Mkurugenzi Mtendaji wa TCB, Adam Mihayo amesema lengo la benki hiyo ni kuhakikisha kwamba wateja wanafikiwa na kunufaika na huduma za mradi wa SGR kupitia mawakala walioenea nchi nzima na uwezo mkubwa wa programu ya TCB Popote, wanamwezesha kila mmoja kujionea urahisi na uhakika wa usafiri wa kisasa.
Aidha, Mihayo ameeleza kuwa sambamba na hilo, benki ilishinda zabuni ya kutoa huduma za ukusanyaji wa nauli kwa njia za kidijiti ikiwemo kupitia mashine za kukatia tiketi (Ticket Vending Machine) pamoja na programu ya simu ya TCB Popote inayomwezesha mteja kujifungulia akaunti kwa kiasi cha 1,000/- tu, inarahisisha ukataji wa tiketi za SGR mahala popote nchini.
Mihayo aatika kuwezesha mfumo kufanya kazi kwa ufanisi, Benki ya TCB imezindua mfumo wa malipo wa QR code kwa abiria ili kuwawezesha kutumia mfumo wa PoS bila kuhitaji intaneti kuzuia makosa ya kimfumo.
Aidha, ubunifu wa mfumo wa kimawasiliano unaotumia akili mnemba kupitia mtandao wa WhatsApp unawezesha upatikanaji wa huduma za SGR kwa urahisi na kwamba , makusanyo ya manunuzi ya tiketi yameunganishwa na mfumo wa GePG ili kuendelea kujenga pato la nchi.
Akihutubia katika uzinduzi huo jijini Dodoma, Rais Samia aliuelezea mradi huo kuwa kielelezo cha maendeleo makubwa ya kimiundombinu na ya taifa kwa ujumla
Mkuu huyo wa nchi alibainisha kuwa wa mradi wa SGR ni hatua muhimu katika kutimiza ndoto ya kuwa na miundombinu ya usafiri wa haraka, rahisi na wa kuaminika.
Alifafanua kwamba matokeo ya mradi yanaweza yasionekane mapema, lakini lengo la mradi ni kutoa huduma kwa taifa na mchango wake katika kuwezesha biashara za kimataifa na maendeleo ya nchi na kuwa Sehemu ya mradi huu inayoendelea kujengwa kuelekea Kigoma mpakani mwa nchi za Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo inaonyesha namna mradi huu utakavyonufaisha uchumi wa nchi hasa sekta ya utalii.
Benki ya TCB imepewa heshima kuwa benki mdau namba moja katika mradi huu wa kimageuzi kwa kuwezesha mchakato wa kuagiza vichwa vya treni na mabehewa ya SGR na kutoa mikopo kwa wakandarasi wa Yapi Merkezi.
Deprecated: htmlspecialchars(): Passing null to parameter #1 ($string) of type string is deprecated in /home/habarileoacc/public_html/wp-includes/formatting.php on line 4720