Teknolojia kukabiliana na moto wa misitu

SERIKALI imewekeza katika teknolojia za kisasa za magari na satelite katika kukabiliana na moto unapotokea kwenye misitu.

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Misitu Tanzania (TFS), Profesa Dos Santos Silayo amesema hayo katika Maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (DITF).

Profesa Silayo amesema kupitia teknolojia ya setelite moto unapotokea unaonekana mapema kabla ya kushika kasi na kwenda kuushambulia.

“Tunauona na kutoa taarifa kwa njia za kijitali za simu na kompyuta,” amesema.

Amesema pia TFS imeongeza kasi katika kutoa elimu kwenye maeneo mbalimbali ambayo yamekuwa na changamoto ya moto na kuitaja mikoa ya Kusini na Magharibi.

“Tumeanzisha vikundi vya kupambana na moto kwenye vijiji, tunawafanyia mafunzo vijana na kuwatengenezea makundi na kuwapa shughuli mbadala wawe na utayari na uwezo wa kupambana na moto unapotokea,” amesema.

Pia vijana hao waweze kuzuia moto kwa haraka pindi unapotokea ili usisambae.

Amesema kumekuwa na changamoto kubwa za mabadiliko ya tabia nchi kwa kuwa vipindi vya ukame vinakuwa virefu Zaidi wakati mwingine havitabiriki na kusababisha maeneo mengi kuwa na ukame wa muda mrefu.

Ameeleza kwa miaka ya karibuni kumekuwa na ongezeko la matukio ya moto kwenye maeneo ya makazi ya watu wanapofanya shughuli za kusafisha mashamba kwa ajili ya kilimo.

Ameeleza wananchi wamekuwa na mazoea ya kusafisha maeneo yao kwa kutumia moto.

Habari Zifananazo

6 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button