Teknolojia ya akili mnemba kudhibitiwa
UINGEREZA : SERIKALI ya Uingereza imeungana na Umoja wa Ulaya na Marekani kutia saini mkataba wa kwanza wa kimataifa kuhusu matumizi ya teknolojia ya akili mnemba lengo ni kutaka mataifa mengine yaweze kujilinda na teknolojia hiyo dhidi ya hatari zinazoweza kujitokeza.
Mkataba huu utakuwa wa kwanza kimataifa unaofungamana kisheria kuhusu teknolojia, ambao umekubaliwa na Shirika la haki za binadamu la Baraza la Ulaya. SOMA : WATEHAMA Tanzania kujadili teknolojia ya akili mnemba
Hatahivyo muongozo wa mkataba huu utazilazimisha nchi kufuatilia maendeleo ya teknolojia ya akili mnemba na kuhakikisha teknolojia hiyo inasimamiwa na kuwekewa sheria kali dhidi ya matumizi mabaya ya teknolojia hiyo.
SOMA : Viongozi wa dunia wakutana Seoul kuijadili Akili ya Kubun