TET, Taasisi ya Aga Khan wapanda miti kuhimiza utunzaji mazingira

DAR-ES-SALAAM : TAASISI ya Elimu Tanzania (TET) kwa kushirikiana na Agha Khan Foundation, leo imepanda miti zaidi ya 200 katika eneo la Makao Makuu ya TET, jijini Dar es Salaam, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Miaka 50 ya taasisi hiyo.

Zoezi hilo lililolenga kuanzisha msitu-bustani, limejikita katika kuelimisha na kuchochea utunzaji wa mazingira na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

Akizungumza katika tukio hilo, Mkurugenzi Mkuu wa TET, Dk. Aneth Komba, amesema taasisi hiyo imeweka mazingira kuwa sehemu muhimu katika maboresho ya mitaala ya elimu.

“Katika mtaala mpya wa mwaka 2023, somo la Jiografia limewekwa kuwa la lazima ili kuwajengea wanafunzi uelewa kuhusu umuhimu wa mazingira,” amesema.

Kwa upande wake, Mkuu wa Programu wa Agha Khan Foundation Tanzania, Carolyn Mlewa, amesema miti hiyo 200 yenye aina 25 tofauti, ikiwemo ya kivuli, dawa, matunda na miti pori, imepandwa kama ishara ya dhamira ya pamoja kulinda mazingira.

Naye Msimamizi wa Mradi wa Mazingira wa TET, Japhet Wangwe, amesema upandaji huo ni hatua ya kuunga mkono juhudi za kitaifa za kuhifadhi mazingira na viumbe hai.

SOMA: Samia, Mwinyi wamuomboleza Aga Khan IV

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button