TGNP yajadili ukombozi wa mwanamke

DAR ES SALAAM: Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) umeadhimisha Siku ya Wanawake Duniani kwa kukutanisha wadau kutoka sekta mbalimbali kwa lengo la kujadili namna ya kumkomboa mwanamke kiuchumi, kupambana na unyanyasaji wa kijinsia pamoja na vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake.

Maadhimisho hayo yamefanyika jijini Dar es Salaam na yanatarajiwa kuendelea kwa kipindi cha mwezi mmoja katika mikoa 15 nchini yenye vituo vya mtandao huo wa TGNP.

Akizungumza katika mkutano huo, Mwenyekiti wa Bodi ya TGNP, Gemma Akilimali, amesema kuna umuhimu kwa wadau na jamii kwa ujumla kushirikiana ili kuhakikisha wanawake wanapata fursa sawa za kiuchumi na kijamii, hatua itakayosaidia kupunguza changamoto zinazowakabili.

Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi wa TGNP, Clara Karanga, ameiomba serikali pamoja na jamii kwa ujumla kuhakikisha wanawake wanashirikishwa kikamilifu katika shughuli za maendeleo ili kufanikisha utekelezaji wa malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo.

Naye Mwanasheria kutoka Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Kajetan Tumaini, amesema kuna umuhimu wa kuendelea kutoa elimu ya sheria kwa jamii ili kupunguza vitendo vya ukatili na unyanyasaji wa kijinsia.

Mshiriki wa mkutano huo Neema Maliwanga amesema maadhimisho hayo yanatoa fursa kwa wanawake kubadilishana uzoefu, kujifunza mbinu mbalimbali za kujikwamua kiuchumi pamoja na kuhamasishana kushiriki kikamilifu katika masuala ya maendeleo ya jamii.

Habari Zifananazo

One Comment

  1. These best sativa gummies were a agreeable surprise. The flavor was greater than expected, which already made them go to bat for b wait in the wings out from a share of functional-style gummies on the market. The packaging looked take a shower, and the serving instructions were carefree to follow, which made the effect determine more polished overall. They fit by nature into a daytime automatic and felt serviceable to hold on hand when something imbecilic and straightforward was needed. Nice configuration, good motif, and an complete product that feels artistically made.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button