Ticha wa Madrasa mbaroni kwa kulawiti watoto 10

JESHI la Polisi mkoani Shinyanga linamshikilia Mwalimu wa Madrasa wa Msikiti wa Mohamed Shunu uliopo kata ya Nyahanga wilayani Kahama mkoani Shinyanga kwa tuhuma za kuwalawiti watoto 10.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga Janeth Magomi amewaeleza waandishi wa habari kuwa watoto hao walikuwa wakipata mafundisho katika madrasa ya msikiti huo.

Mtuhumiwa, kwa nyakati tofauti alikuwa akiwarubuni watoto kwa kuwapa  Sh.1500 kisha kuwafanyia ukatili huo. “Ni kweli tukio hili lilitokea wiki iliyopita ambapo sisi  tulifika eneo la tukio na kuwaona watoto na tumemkamata mtuhumiwa mkoani Kigoma alikokuwa amekimbilia,” alisema Magomi.

Advertisement

Magomi alitoa wito kwa wananchi wawe wanatoa taarifa haraka kwenye vyombo vya sheria ili kuwanusuru watoto.

Mwenyekiti wa mtaa wa shunu, Joseph Kaliwa alisema alipata taarifa ya tukio la kulawitiwa watoto hao, hali iliyomfanya kuitisha kikao cha wazazi wa watoto waliofanyiwa ukatili.

Kaliwa alisema walishirikiana na ofisa ustawi wa jamii wilayani humo kisha wakawapeleka hospitali kwa ajili ya kupatia dawa itakayosaidia kuwakinga na magonjwa.

 

 

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *