TikTok yapata mnunuzi, majina yahifadhiwa

WASHINGTON DC : RAIS wa Marekani, Donald Trump, amesema kuna kundi la wawekezaji wenye uwezo mkubwa kifedha walioko tayari kununua mtandao wa kijamii wa TikTok, lakini amesema hatataja majina yao kwa sasa.

Akizungumza na kituo cha televisheni cha Fox News siku ya Jumapili, Trump alisema: “Nitawaambia kuhusu hilo baada ya wiki mbili.” SOMA : TikToker atupwa jela miezi sita

Mtandao wa TikTok unamilikiwa na kampuni ya teknolojia kutoka China, ByteDance, na hatua ya kuuza jukwaa hilo bado inasubiri idhini ya serikali ya China, ambayo haijatoa tamko lolote hadi sasa.

Mwezi Aprili 2024, Bunge la Marekani lilipitisha sheria inayotaka TikTok kuuzwa kwa kampuni ya Marekani. Sheria hiyo inaelekeza kuwa endapo TikTok haitauzwa, basi itapigwa marufuku nchini Marekani kuanzia Januari 19, 2025.

Wabunge wa Marekani wanadai kuwa TikTok inaweza kutumika kupeleka taarifa za watumiaji wa Marekani kwa serikali ya China, hali ambayo wanaiona kuwa tishio kwa usalama wa taifa.

Hata hivyo, TikTok imeendelea kukanusha madai hayo na kusisitiza kuwa haijawahi kushirikiana na mamlaka ya China katika ukusanyaji au usambazaji wa taarifa za watumiaji wake.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button