HAI, Kilimanjaro – KATIBU Tawala mkoa wa Kilimanjaro, Tixon Nzunda amefariki dunia leo baada ya kupata ajali wilayani Hai mkoani Kilimanjaro akiwa na Dereva wake, Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, Nurdin Babu amethibitisha.
Nzunda amewahi kushika nyadhifa kadhaa serikalini ikiwa ni pamoja na Naibu Katibu Mkuu katika Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo), na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu).