TMDA yakamata sigara bandia

shehena la sigara bandia kanda ya ziwa magharibi

MAMLAKA ya Dawa na Vifaa tiba Tanzania (TMDA) kanda ya ziwa magharibi, imekamata sigara bandia aina ya SuperMatch yenye thamani ya Shilingu bilioni 1.8

Taarifa iliyotolewa leo Jumatano Septemba 28, 2022 na Meneja wa kitengo cha Uhusiano TMDA, Gaudensia Simwanza imeeleza walipokea taarifa kutoka kwa Mamlaka ya Mapato Shinyanga.

“TMDA kanda ya ziwa magharibi  baada ya kupokea taarifa ya kontena lenye bidhaa za tumbaku lililozuiliwa katika ofisi ya TRA Shinyanga, imebaini sigara hizo ni bandia na zimeingizwa nchini kutoka nchi jirani ya Kongo, kuna makasha 2200 yenye thamani ya shilingi bilioni 1.8” Amesema

Advertisement

Amesema makasha hayo yana uzito wa tani 13.2  na kwamba kazi hiyo imefanikiwa kwa kushirikiana  kwa karibu  na MCIE.

Sigara bandia ambazo zimekatwa kanda ya ziwa magharibi aina ya SuperMatch

“Lakini cha kujiuliza zimepitaje mipakani na tunao wakaguzi huko? Hatua zaidi zinaendelea kuchukuliwa na mzigo huu umezuiliwa,” amesema Simwanza.