KAMATI ya Olimpiki Tanzania (TOC), imesema kuwa inaanza maandalizi mapema ili kuiwezesha Tanzania kupata medali katika Michezo ya Olimpiki ya 33 itakayofanyika Paris, Ufaransa mwaka 2024.
Makamu wa Rais wa Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC), Henry Tandau alisema hayo leo wakati akimkaribisha mgeni rasmi, ambaye ni Rais wa TOC, Gulam Rashid kufungua Mkutano Mkuu wa kamati hiyo mjini hapa.
Tandau alisema kuwa maandalizi ya kushiriki michezo hiyo inaanza mapema, ili kuhakikisha nchi inapata medali ya aina yoyote katika Michezo ya Olimpiki ya Paris 2024.
Tandau alisema kuwa tayari TOC imeandaa mashindano maalumu ya michezo ya riadha, ndondi na judo kwa ajili ya kupata wachezaji watakaofuzu kushiriki michezo hiyo ya Olimpiki.
Alisema kuwa mashindano hayo yafanyika kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa na ule wa Ndani wa Taifa kuanzia Desemba 17 hadi 18 na wachezaji watakaofikia viwango wataingia kambini na kupata mafunzo maalumu ndani na nje ya nchi, ili kufikia viwango vya kushiriki Michezo ya Olimpiki.
Katibu Mkuu wa TOC, Filbert Bayi akizungumza katika mkutano huo, alisema kuwa vyama vingi vya michezo vinashindwa kuandaa mashindano yao ya taifa.
Alisema pia vyama vingi havina Kamisheni za Wachezaji na badala yake wamekuwa wakipeleka viongozi wa vyama katika mikutano ya Kamisheni ya Wachezaji.
Thank you for your sharing. I am worried that I lack creative ideas. It is your article that makes me full of hope. Thank you. But, I have a question, can you help me?