Tosci yatakiwa kuweka mkazo ukaguzi mbegu,mashamba

NAIBU  Waziri wa Kilimo, Anthony Mavunde ameitaka Taasisi ya Uthibiti na Udhibiti wa Mbegu Tanzania (TOSCI) kuhakikisha inaweka mkazo mkubwa kwenye ukaguzi wa mashamba ya mbegu ili kuhakikisha mbegu zinazosambazwa kwa wakulima kuwa ni mbegu bora zitakazoleta leta tija katika  uzalishaji.
 Mavunde ameyasema hayo leo Machi 15,2023 alipotembelea na kukagua utekelezaji wa majukumu wa TOSCI.
Amesema  tasnia muhimu haitaweza kujitosheleza kwa chakula au kufikia malengo yaliyowekwa katika uzalishaji wa mazao pasipo kuwa na uhakika wa mbegu bora.
“Serikali yenu inayoongozwa na mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan  itaendelea kuongeza uwekezaji kwenye utafiti na uzalishaji wa mbegu bora nchini ili tuweze kufikia malengo makuu ya kukuza kilimo kwa asilimia 10 ifikapo mwaka 2030.’Amesema Mavunde
Amesema ni lazima TOSCI itimize jukumu la kubwa la kuhakisha mashamba ya uzalishaji ya mbegu yanakaguliwa,kwasababu wao ndio wenye dhamana ya uthibiti na udhibiti wa mbegu hapa nchini.
“Rai yangu kwenu ni kuimarisha ukaguzi ili mkulima  anufaike na mbegu bora.”
Amesema serikali itahakikisha inaendelea kuwekeza katika vifaa na miundombinu bora ili kurahisisha jukumu hilo sambamba na kuwajengea uwezo watumishi wa TOSCI ili waweze kutekeleza majukumu yao kiufanisi kwa kufuata misingi ya utaalamu wa kazi yao.
 Serikali kupitia Wizara ya Kilimo itaendelea kutafuta fursa mbalimbali nje ya nchi na kuwawezesha Wataalam wengi zaidi wa TOSCI kwenda kujifunza ili kuleta manufaa zaidi kwa tasnia ya mbegu na Taifa kwa ujumla.
Ninawapongeza sana kwa kazi kubwa ya maboresho ya maabara na ujenzi wa maktaba,ni imani yangu k ofwamba hatua hii itaongeza zaidi ufanisi katika kutekeleza majukumu yenu”Alisema Mavunde
Naye Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya TOSCI, Patrick Ngwediagi alibainisha mafanikio ya Taasisi yake ikiwemo kuongezeka kwa mbegu zilizothibitishwa ubora, kupungua kwa mbegu feki kunakotokana na matumizi ya lebo za kielektroniki na kuongeza uzalishaji wa ndani wa mbegu kulinganisha na zinazoagizwa

Habari Zifananazo

Back to top button