TPDC yakagua mitambo ya gesi

SHIRIKA la Maendeleo ya Petrol Tanzania ( TPDC) limekagua mitambo ya utafiti wa mafuta na gesi kwa njia ya mitetemo ardhini ya Kampuni ya Ukandarasi ya Africa Geophysical Services (AGS) na kuridhishwa nayo.

Akizungumza wakati wa kikao cha kwanza kati ya shirika hilo na Kampuni ya AGS, mjini Kibaha, mkoani Pwani, Meneja wa Mradi wa Utafiti wa Mafuta na Gesi katika kitalu cha Eyasi Wambere uliopo katika Bonde la Ufa la Afrika Mashariki, Sindi Maduhu, alisema mitambo hiyo inakizi vigezi vya utafiti huo.

Advertisement

Amesema serikali imetoa zaidi ya Sh billion 8 kwa ajili ya utekelezaji wa mradi huo kwa awamu ya nne na kwamba utatekelezwa katika mikoa mitano.

“Mradi ulishaanza ambapo kwa sasa ni awamu ya nne ambayo itahusisha utafutaji wa mafuta kwa njia ya mitetemo na kikao hivyo tumefanya kikao Cha kwanza na wakandarasi hawa wa Africa Geophisical Services (AGS) kwa ajili ya ukaguzi wa mitambo ya kazi na tumejiridhisha wanavifaa vya kutosha Kwa kazi hii.” alisema Wambere.

Aidha alisema mradi huo unatrajiwa kumchukua muda wa miezi mitatu hadi miezi sita na kwamba baada ya awamu hiyo kukamilika wataingi katika awamu ya tano ambayo itakuwa ni kumchukua takwimu na kuzitafsii.

Kwa upande wake mkandarasi anayetekeleza mradi huo wa kampuni ya Africa Geophisical Services (AGS), Salim Ajib, alisema, anaishukuru serikali Kwa kuwaamini na kuwapa frusa kama wakandarasi wazawa na kwamba wanategemea kufanya kazi hiyo kwa ufanisi na kwa muda uliopangwa.

“Serikali imetuamini na nitahakikisha tunaifanyakazi hii Kwa ufanisi zaidi ili serikali iendelee kutuamini wakandarasi wazawa kwani jambo hilo linasaidia kuongeza mapato yetu na kutoa ajira kwa vijana wengine wakitanzania.” aliongeza Wambere.