TRA Dodoma yawafariji wenye uhitaji

DODOMA: MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Dodoma imetembelea kaya za watu wenye ulemavu wa macho kwa lengo la kutoa faraja, upendo na kuwajengea matumaini kuelekeza sikukuu za pasaka.

Ziara hiyo fupi imefanyika leo Aprili 2,2026 katika eneo la Matembebora wilayani Chamwino ikiongozwa na Meneja wa TRA Mkoa wa Dodoma, Pendolake Elinisafi akiongozana na Meneja Msaidizi Huduma kwa Walipa Kodi, John Njau, pamoja na watumishi wengine.

Akizungumza katika ziara hiyo, Elinisafi amesema watu wenye ulemavu wa macho ni sehemu ya jamii inayothaminika, hivyo ziara hiyo imeacha ujumbe wa upendo na mshikamano, ikionesha dhamira ya TRA ya kuendelea kugusa maisha ya jamii sambamba na majukumu yake ya ukusanyaji wa mapato.

Akizungumza kwa niaba ya wanakaya hao Mwenyekiti, Yeledi Cheleso ameishukuru TRA na ujumbe wake kwa moyo wa kujali na msaada walioutoa, akieleza kuwa hatua hiyo imeongeza faraja na kuwapa nguvu mpya ya kuendelea na maisha.

Kwa upande wake, Ofisa Maendeleo ya Jamii, Elizabeth ameipongeza TRA kwa kuendeleza mshikamano na jamii, akibainisha kuwa juhudi hizo zinaimarisha ushirikiano kati ya taasisi na wananchi, hususani kwa makundi yenye uhitaji maalumu.

Habari Zifananazo

2 Comments

  1. JOIN US Everybody can earn 250/h Dollar + daily 1K… You can earn from 12000-16700 Dollar a month or even more if you work as a part time job…It’s easy, just follow instructions on this page, read it carefully from start to finish… It’s a flexible job but a good earning opportunity. tab for more detail thank you……..
    .
    This is my main concern…………………… http://Www.Cash54.Com

  2. I just came across this amazing way to earn $11,000-$15,000 a month online! No selling, no struggle—just a simple system that anyone can follow. Mia Westbrook did it, and so can you! Don’t miss out on this life-changing opportunity……….
    .
    This is what I do…………………… http://Www.Payathome9.Com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button