TRA yakusanya Sh bilioni 6 robo ya kwanza Kahama

MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa kikodi Kahama umefanikiwa kukusanya kukusanya Sh bilioni 6.59 sawa na ufanisi wa asilimia 125 kwa kipindi cha robo ya kwanza ya mwaka kuanzia Julai hadi Novemba mwaka wa fedha 2023/2024.

Hayo yalisemwa jana na kaimu meneja kutoka mamlaka hiyo, Wisaka Kamwamu wakati wa kilele cha maadhimisho ya wiki ya shukrani kwa mlipa kodi huku mgeni rasmi akiwa Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mboni Mhita.

Advertisement

Kamwamu alisema malengo ya makusanyo yalikuwa ni Sh bilioni 7.2 kwa kipindi hicho huku akieleza biashara ya magendo ndiyo imekuwa ikirudisha nyuma maendeleo ya ulipaji wa kodi kwa ufanisi.

“Shughuli ya ukusanyaji wa kodi ni endelevu ina hitaji uimara kwa kila siku na wafanyabiashara wanapouza watoe risiti na wateja wadai risiti kwani usipodai risiti unarudisha nyuma jitihada za serikali kufikia malengo yake”alisema Kamwamu.

Naibu mkurugenzi wa fedha kutoka TRA makao makuu Anna Mdeme alisema wafanyabiashara waache kuficha taarifa zao ili kuweza kukusanya mapato,hivyo huduma bora zenye uwajibikaji ndiyo msingi bora wa kulipa kodi na mmamlaka imeeleza kutoa elimu zaidi ili kuleta uwajibikaji kwa walipa kodi.

Mdeme alisema kuanzia mwaka 2022/2023 mwezi Julai hadi Septemba ambayo ni robo ya kwanza ya mwaka wa fedha wamekusanya Sh trilioni 6.58 sawa na ufanisi asilimia 97.53 makusanyo hayo ni ongezeko kubwa la asilimia 11.05 ila mwaka uliopita walikuwa na ongezeko la asilimia 8.

 

Mkuu wa wilaya ya Kahama Mboni alisema kuna mbinu inayotolewa kwa baadhi ya wafanyabiashara kwa wateja wao kuwa ukitaka risiti ni sh 120,000 na usipochukua risti ni sh 80,000 hiyo mbinu kutaka kukuvunja moyo wa mteja ili asichukue risiti na yeye kukwepa ulipaji wa kodi kwa njia hiyo.

Kauli mbiu “Kodi yetu maendeleo yetu tuwajibike” ili kuwa na kumbukumbu sahihi za baishara yako lazima ujue kodi inayotozwa hivyo utunze kumbukumbu na hapo utalipa vizuri kuliko wasiotunza kumbukumbu”.alisema Mhita.

Mwenyekiti wa chemba ya wafanyabishara, viwanda na kilimo (TCCIA ) Wilaya ya Kahama Charles Machali alisema kutunukiwa vyeti wafanyabiashara na kuongezeka mapato ni jitihada zilizofanywa na wao katika kuhamasisha kuwa kodi ni maendeleo na ndiyo maana kila kukicha biashara inaanzishwa.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *