WASHINGTON, D.C: RAIS wa Marekani, Donald Trump, amethibitisha kuwa atatangaza ushuru wa 25% kwa biashara ya chuma na aluminium zote zinazoingia nchini Marekani, hatua inayotarajiwa kuwa na athari kubwa kwa biashara kati ya Marekani na Canada.
Katika mazungumzo na waandishi wa habari alipokuwa akisafiri kutoka eneo la mapumziko la Mar-a-Lago huko Florida hadi New Orleans kwa ajili ya michezo ya Super Bowl, Trump alisema kuwa hatua hii ni jibu kwa nchi zinazotoza ushuru kwa bidhaa za Marekani.
“Ikiwa wanatutoza, sisi pia tutawatoza,” alisisitiza, huku akiongeza kuwa atatoa maelezo zaidi kuhusu mataifa yatakayolengwa na ushuru huo baadaye.
Canada na Mexico ni miongoni mwa washirika wakubwa wa Marekani katika biashara ya chuma na aluminium, na Canada ikiwa ni msambazaji mkuu wa aluminium kwa Marekani.
Hatua hii inatumiwa na Trump kama sehemu ya kuongeza nguvu katika majadiliano ya kibiashara, huku akitaka kulinda sekta za ndani za Marekani.
Wakati wa muhula wake wa kwanza, Trump alianzisha ushuru wa 25% kwa chuma na 10% kwa aluminium kutoka kwa mataifa kama Canada, Mexico, na Umoja wa Ulaya.
Ingawa Marekani ilikubaliana na Canada na Mexico na kumaliza ushuru huo, ushuru kwa bidhaa za Umoja wa Ulaya ulidumu hadi 2021. SOMA: Serikali yapewa ushauri athari uamuzi wa Trump
Rais Trump amethibitisha kuwa atatangaza ushuru kwa “kila mtu” anayeshiriki katika biashara ya chuma na aluminium, akisisitiza kuwa chuma chochote kinachoingia Marekani kitapata ushuru wa 25%.
Hatua hii mpya inayotarajiwa kutangazwa Jumatatu itakuwa na athari kubwa kwa biashara ya kimataifa, huku mataifa mengi yakihofia kwamba itasababisha mvutano zaidi katika masuala ya kibiashara duniani.
My family members all the time say that I am killing my
time here at web, except I know I am getting familiarity
all the time by reading thes good posts.
Os brasileiros actores gostam de se desafiar! As anterior impressões do sítio Web jogos indústria são
as de casino máquinas. Estes desporto apresentam técnica, ótimo sorte, rácios,
e muita emoção. À medida que o jogo progride, os participantes são obrigados a apostar no compostos pré-jogo crenças à medida que
o multiplicador reforça. Quando as coisas estão a correr bem, porque um
incidente está prestes a ocorrer, o objetivo
é ganho. https://groups.google.com/g/sheasjkdcdjksaksda/c/6uprFNJrvwI