Trump, Putin kukutana Alaska wiki hii

ALASKA : VIONGOZI wa Umoja wa Ulaya (EU) wamemuomba Rais wa Marekani, Donald Trump, kuhakikisha usalama wao katika mkutano wa kilele na Rais wa Urusi, Vladimir Putin, unaotarajiwa kufanyika wiki hii  utakaojadili vita vya Ukraine.

Viongozi hao wameeleza kuwa wanatarajia kikao hicho kiwe na ushawishi wa kumaliza mgogoro wa Ukraine. Mkutano huo unatarajiwa kufanyika Ijumaa, ingawa viongozi wa EU hawajalikwa kushiriki. Hadi sasa haijafahamika iwapo Ukraine itahudhuria kikao hicho kitakachofanyika Alaska.

SOMA: Ulaya Kuijenga Upya Ukraine

Awali, Trump alisema anataka kukutana na Putin ili kubaini kama ana nia ya kweli ya kumaliza vita hivyo, ambavyo sasa vipo katika mwaka wake wa nne. Kauli ya Trump kwamba Ukraine inapaswa kuyaachia maeneo yake kwa Urusi, huku Urusi pia ikubali kubadilishana maeneo, kauli ambayo iliwashtua washirika wake wa Ulaya.

Habari Zifananazo

One Comment

  1. 13win tự hào là nhà cái cá cược trực tuyến hàng đầu tại Việt Nam, sở hữu kho game đồ sộ với hơn 500 tựa game cá cược hấp dẫn. 13WIN thường xuyên tung ra các khuyến mãi hấp dẫn tri ân người chơi mỗi ngày. Tham gia ngay!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button