Trump apanga kukutana Vladimir Putin

MAREKANI : RAIS wa Marekani, Donald Trump, ametangaza kuwa atazungumza na Rais wa Urusi, Vladimir Putin, kesho Jumanne kuhusu juhudi za kumaliza vita vya Ukraine.

Trump amesema mazungumzo ya pande hizo mbili tayari yanaendelea, na kugawana mali kadhaa ni sehemu ya majadiliano hayo. SOMA: Trump kutangaza ushuru wa 25% kwa biashara ya chuma na aluminium

“Tutazungumza kuhusu ardhi na mitambo ya umeme, hiyo ndiyo mada kuu,” alisema Trump, akisisitiza kuwa pande zote mbili tayari zimejadili masuala haya kwa kina.

Hapo jana, maafisa wa Marekani walieleza matumaini ya kufikiwa kwa makubaliano ya kusitisha mapigano kati ya Ukraine na Urusi katika wiki chache zijazo.

Washington ilipendekeza kusitishwa kwa vita vya miaka mitatu kupitia mazungumzo ya Saudi Arabia, pendekezo ambalo Ukraine limekubali, huku Urusi ikiwa bado haijatoa jibu rasmi kuhusu pendekezo hilo.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button