MAREKANI : RAIS mteule wa Marekani, Donald Trump, na Rais wa Urusi, Vladimir Putin, wanatarajiwa kufanya mazungumzo kwa njia ya simu hivi karibuni.
Mshauri wa usalama wa taifa, Mike Waltz, atakayechukua wadhifa huo mara tu Trump atakapoingia madarakani, amethibitisha kuwepo kwa mpango huo.
“Bado hatujaweka mpango kazi kamili wa mazungumzo hayo. Tunaufanyia kazi, lakini mazungumzo kati ya Trump na Putin yanatarajiwa kufanyika katika siku kadhaa au wiki zijazo,” alisema Waltz.
Trump, atakayekuwa Rais wa Marekani kuanzia Januari 20, anajipambanua kama msuluhishi katika vita vinavyoendelea kati ya Urusi na Ukraine. SOMA: Putin yuko tayari kukutana na Trump