TSN yatoa majaji wawili kati ya 12 Tuzo za EJAT

WATUMISHI wawili wa Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) wameteuliwa na Baraza la Habari Tanzania (MCT) kuwa majaji wa Tuzo za Umahiri wa Uandishi wa Habari Tanzania (EJAT) makala ya 16.

Jumla ya majaji 12 wametangazwa leo Aprili 13 jijini Dar es Salaam na Katibu Mtendaji wa MCT, Ernest Sungura, ambapo amemtaja Mkurugenzi Mtendaji wa TSN, Asha Dachi, pamoja na Mwandishi Mwandamizi wa kampuni hiyo, Sauli Giliard, kuwa miongoni mwa majaji wa tuzo hizo kongwe nchini Tanzania.

Mara baada ya kutajwa kwa majaji hao, Wakili Ally Kileo aliwaapisha kwa kuzingatia Katiba ya Tanzania, akisisitiza kuwa kiapo hicho ni takwa la kisheria chini ya Sheria ya Viapo na Tamko la Kisheria, Sura ya 34 ya mwaka 1967 iliyofanyiwa maboresho mwaka 2023.

Baada ya zoezi hilo, Sungura aliwataka majaji hao kuzingatia weledi katika utekelezaji wa majukumu yao kwa kuongozwa na vigezo vya EJAT, sambamba na kuzingatia ubora wa kazi, tija na maslahi ya umma. “Amesema, tuzo hizo zitazingatia zaidi tija kwa jamii ikizingatiwa kuwa mwenendo uliopo sasa kuna taswira hasi kwa jamii hivyo kigezo cha tija ni kigezo cha mwisho zaidi baada ya vigezo vya kitaaluma na maadili,” amesisitiza Sungura.

Ameongeza kuwa jamii inataka kuona habari zinazoonesha uwajibikaji na ufumbuzi kwa jamii kama kufichua mafisadi, kusukuma maendeleo na kadhalika. Amesisitiza kuwa tuzo hizo ni muhimu kwa kuiheshimisha tasnia ya habari, kuongeza wasifu wa mshindi pia kumfungulia zaidi milango ya fursa.

Kwa upande wake, Jaji mteule wa tuzo hizo, Sauli Giliard amesema ni heshima kubwa kwake kuwa miongoni mwa majaji wazoefu katika tasnia ya habari nchini, na ameahidi kutumia uzoefu wake kusimamia maadili na kuiwakilisha vyema TSN. Ikumbukwe, Sauli, ameshiriki mara kadhaa na kushinda katika tuzo hizo ambapo mwaka 2021 aliwahi kunyakua tuzo hizo katika kipengele cha umahiri kwenye Habari za mazingira.

Majaji wateule, wanaendelea na semina mabalimbali huku wakitarajiwa kujifungia kutafuta waandishi mahiri zaidi katika Tuzo za EJAT msimu wa 16 zitakazofanyika Mei 29 mwaka huu. SOMA: Waandishi 91 wateuliwa tuzo za EJAT

Habari Zifananazo

3 Comments

  1. l Get paid over $110💸 per hour working from home. l never thought I’d be able to do it but my buddy makes over $22174💸 a month doing this and she convinced me to try.Single Mom Reveals How She Earns 88k/Yr Working 10 Hrs/Week From Home The possibility with this is endless____ https://FindJobs1.Site

  2. thisis a fantastic article, really nice created, i enjoy reading it, i will be back to check out for latest update, keep up the good work and applause. ng.yandaz.com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button