DAR ES SALAAM: Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) ikishirikiana na wadau wa utalii imekuja na programu maalum ya kuhamasisha utalii wa ndani iitwayo “LIKIZO TIME” inayoanza desemba 3 hadi januari 5, 2024.
Programu hiyo imeandaliwa kipindi cha kuelekea msimu wa mapumziko ya mwisho wa mwaka ambapo kutakuwa na mashindano kupitia mitandao ya kijamii (social media challenges) na vyombo vya habari, washindi watapata zawadi ya kutembelea vivutio vya utalii pamoja na kukaa kwenye hoteli mbalimbali bila gharama.
Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Damasi Mfugale amesema programu hiyo itaendelea katika sikuku zote, ili kuwajengea Watanzania tamaduni ya kutembelea vivutio vya utalii vya ndani.
“Na sisi hatuishi tu kipindi cha krismas sikuku zote, Pasaka, kipindi cha Eid, Maulid, sikuku zote, za kitaifa na za kiimani tutahakikisha watanzania wanaende kutembelea vivutio vyetu” amesema Damasi Mfugale.
Nae Mkurugenzi wa Tanzania House of Talent (THT), Kemi Mutahaba akiwa kama moja wa wadau wa utalii na kampeni hiyo ameeleza nia yao ya kutumia vipaji vya vijana kuhamasisha watanzania,kupitia utengenezaji wa maudhui na matangazo ili kukuza hi kampeni ya LIKIZO TIME.
Comments are closed.