TTCL kuimarisha usalama sekta ya mawasiliano

SHIRIKA la Mawasiliano Tanzania (TTCL) limesema litahakikisha linakuwa lango la usalama wa kitaifa wa kielektroniki kwa kuimarisha usalama wa sekta ya mawasiliano.

Kadhalika limesema litahakikisha linaimarisha huduma za kimtandao za E-serikali kwa kukaribisha miundombinu na huduma muhimu za Tehama ( ICT), kwa kuwa ni kitovu cha mawasiliano nchini.

Mkurugenzi wa Biashara wa TTCL Vedastus Mwita amesema hayo katika kongamano la Connect 2 Connect (C2C), linalofanyika Zanzibar na kuongeza kuwa, shirika hilo linatoa huduma ya intaneti ya kiwango cha juu katika kongamano hilo ili kuwawezesha wadau kuperuzi kwa uharaka na urahisi zaidi.

Amesema huduma hiyo ya intaneti imefanikiwa kutokana na uwepo wa miundombinu imara inayotolewa na TTCL.

Amesema, “TTCL si tu kama mtoa huduma za mawasiliano ya simu bali kama mhusika mkuu aliyepewa mamlaka ya kupanga, kujenga, kuendesha na kudumisha miundombinu ya kimkakati ya mawasiliano ya simu, ambayo inaweza kubadilika kulingana na mabadiliko ya kisasa ya kiteknolojia na miundombinu hiyo imeundwa ili kuendana na mwingiliano wa waendeshaji ndani na nje ya Tanzania.

Aidha amesema kwa sasa TTCL imefanya mabadiliko makubwa katika Kuboresha utoaji wa huduma ambapo imehakikisha miundombinu ya Mawasiliano ya simu kupitia Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano (NICTBB) umeboreshwa ambapo kwa sasa unapakana na nchi 8 ikiwemo Kenya, Congo, Rwanda,Burundi, Malawi, Uganda.

Mwita amesema TTCL inahakikisha uhifadhi data kwa kutoa suluhisho na vifaa vya kutunza data kwa kupitia kituo cha kutunza data kimtandao (NIDC) kilichoidhinishwa na ISO.

Amesema pamoja na hilo TTCL inahakikisha inakuwa ndio lango la huduma za E-serikali kwa kukaribisha miundombinu na huduma muhimu za ICT, Lango la usalama wa kitaifa wa kielektroniki kwa kuimarisha usalama na usalama wa sekta ya mawasiliano.

Kongamano hilo la siku mbili limeanza leo, Septemba 6-7, 2023 linawakutanisha wadau zaidi ya 250 wa Tehama ili kuelezana ukuaji wa teknolojia, fursa mbalimbali za kibiashara pamoja na ushirikano wa kibiashara.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
3 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
IsabellaChris
IsabellaChris
20 days ago

Everybody can earn 500 dollars daily. Yes! you can earn more than you think by working online from home. I have been doing this job for like a few weeks and my last week payment was exactly 30,000 dollars.
.
.
Detail Here————————————————————–>>>  http://Www.BizWork1.Com

Akamatwa na Madawa
Akamatwa na Madawa
20 days ago

Akamatwa na Madawa ya kulevya kukamatwa na dawa za kulevya kilo 888.08 zilizokuwa zimefichwa ndani ya viatu Vyake.

Capture.JPG
Akamatwa na Madawa
Akamatwa na Madawa
19 days ago

NILICHOKA KUKULEA MWANANGU SERIKALI IMENIONA NILIKUWA NAKUTAMKIA MAMBO YA AJABU AJABU NILIZANI NAHELA, KWA SABABU NYUMBA YANGU HAINA SLING BOARD

NENDA KALELE KWEYE KITUO

AU

SERIKALI KUZINDUA MAKAO MAKUU YA KITAIFA YA WATOTO

Capture.JPG
Back to top button
3
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x