Tume ya mipango, wadau wa maendeleo wakutana Dar

TUME ya Taifa ya Mipango imefanya mazungumzo na wadau wa maendeleo jijini Dar es Salaam kwa lengo la kuimarisha ushirikiano wa maendeleo na kuendeleza mahusiano ya kimkakati.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa kikao hicho, Katibu Mkuu wa Mipango na Katibu Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Mipango, Dk.Tausi Kida amesema mazungumzo hayo yamelenga kujenga uelewa wa pamoja kuhusu vipaumbele vya maendeleo vya Tanzania vilivyoainishwa katika Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano (FYDP IV) na Dira ya Maendeleo ya 2050.
Amesema ushirikiano huo unalenga kuhakikisha kuwa programu za wadau wa maendeleo zinaendana na vipaumbele vya kitaifa vitakavyoimarisha uratibu kati ya Serikali na washirika wake. Hatahivyp amesema hatua hiyo inalenga kuendeleza uwiano sahihi kati ya programu za maendeleo na mipango ya kitaifa.
“Tunalenga kubadilishana mawazo kuhusu maeneo ya ushirikiano na kukubaliana juu ya mbinu zitakazokuza zaidi ushirikiano wetu na kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa FYDP IV na Dira ya 2050,” alisema Dkt Kida. SOMA: Tume ya Mipango yazitaka serikali za mitaa PPP

Naye Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dk. Samwel Shelukindo amesema Tanzania ipo tayari kuendelea kushirikiana na wadau wa maendeleo katika kutekeleza mipango mbalimbali ya maendeleo nchini.
Akiwakilisha Kundi la Wadau wa Maendeleo (DPG), Naibu Mkuu wa Ujumbe wa Ireland Susan Peting amesema Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050 inatoa mwongozo muhimu wa kuongoza Serikali pamoja na wadau wa maendeleo katika kuunda mwelekeo wa maendeleo ya baadaye ya nchi.

Hatahivyo, Peting amebainisha kuwa wadau wa maendeleo wanaendelea kujitolea kufanya kazi kwa karibu na Serikali ili kuhakikisha kuwa programu na mifumo yao ya msaada inaendana kikamilifu na ajenda ya maendeleo ya muda mrefu ya Tanzania.
Katika hatua nyingine, Peting ameishauri Serikali kuendelea kuimarisha utulivu wa kisiasa utakaosaidia kuvutia wawekezaji kuja Tanzania kuwekeza katika mipango mbalimbali ya maendeleo ya nchi.




I am making effectively tirelessly $15k to $20k basically by doing coordinate work at domestic. Multi month once more i have made $45890 from this development. astounding and smooth to do work and standard pay from this can be stupefying. i have propose each last one of you to connect this advance right specifically as moo security and get than full time compensation through take after this affiliation.
:
) AND Great Good fortune.:
)
HERE====)> www.work27.online