DAR ES SALAAM: Rais Samia Suluhu Hassan amesema tangu mwaka 2021 serikali imetekeleza hatua mbalimbali kuboresha afya ya uzazi, afya ya mama na watoto wachanga pamoja na lishe.
Kiongozi huyo wa nchi amesema alipochukuwa madaraka aliahidi kwamba pamoja na kuwekeza katika vituo vya afya na wafanyakazi wa sekta ya afya, pia ataipa kipaumbele afya ya mama na mtoto.
Rais Samia amezungumza hayo katika hafla ya kupokea Tuzo Maalum ya Kimataifa ya The Global Goalkeeper Award kutoka kwa Rais wa Kitengo cha Usawa wa Jinsia kutoka Taasisi ya Gates, Dk Anita Zaidi tukio ililofanyika leo Februari 4, 2025 Dar es Salaam.