‘Tumejiandaa vizuri kuwakabili Azam’

‘Tumejiandaa vizuri kuwakabili Azam’

KOCHA Mkuu wa Simba, Roberto Oliveira Robertinho, amesema kesho wanatarajia kupata upinzani mkali kutoka kwa Azam FC, lakini amekiandaa vizuri kikosi chake kupata pointi tatu.

Akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari, kocha huyo ameeleza kuwa kitu kikubwa kilichokuwa kikiwasumbua ni kuzitumia nafasi wanazotengeneza, lakini kwa maandalizi waliyofanya kuekea mchezo wa kesho anaamini watapata pointi tatu.

“Safu yangu ya ushambuliaji haijafunga bao katika mechi mbili za ligi ya mabingwa hilo ni tatizo, lakini tumeliona hilo na kulifanyia kazi kwenye uwanja wa mazoezi, naamini kesho halitokuwepo, lengo letu ni ushindi,” amesema Robertinho.

Advertisement

Pamoja na kupoteza mechi mbili mfululizo za Ligi ya Mabingwa Afrika, lakini kocha Robertinho amewaomba mashabiki wao kuendelea kuwapa  sapoti wachezaji wao, pamoja na benchi la ufundi kutokana na furaha wanayowapa kila wiki kwenye mashindano mbalimbali wanayoshiriki.