“Tumia mswaki miezi mitatu tu”

DAR ES SALAAM: Daktari bingwa wa kinywa na meno, Josephati Kunji kutoka Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Epiphany iliyopo jijini Dar es Salaam amesema ili mswaki uwe na viwango vinavyotakiwa unatakiwa kubadilisha agalau kila baada ya miezi mitatu.

Akizungumza katika kilele cha maadhimisho ya Siku ya Kinywa na Meno Duniani Machi 20, Dk Kunji amesema mtu ambaye habadilishi mswaki kwa muda huo anakuwa katika hatari ya kupata matatizo ya kinywa na meno.

“Unatakiwa kubadilisha angalau kila baada ya miezi mitatu kwa maana hiyo kwa mwaka unatakiwa kuwa na miswaki minne na kukaa na mswaki mmoja mwaka mzima unakuwa na hatari ya kupata magonjwa ya kinywa na meno,” amesema.
Amesisitiza: “watu wanatakiwa kubadilika na kama unatumia mswaki tayari umeshakuwa mgumu na zile nyuzi zimeshaanza kutoka unakuwa unaumiza fizi na meno yanasugulika tabaka la juu linalolinda hivyo linabaki wazi na litatoboka atapata maumivu.”

Advertisement

Aidha amesema kuna madhara kwa afya ya kinywa na meno pale watu wanapotumia majivu, mkaa, karafuu, sabuni, chumvi na njia zingine zisizo za kitaalamu.

Dk Kunji amesisitiza kuwa njia sahihi ya kutunza meno na kinywa ni kutumia dawa ya meno ambayo ina madini ya floraidi.

“Lakini wengi wanatumia dawa ambazo hazina madini ya floraidi wengine wanatumia mkaa ,wengine majivu na wengine hadi karafuu hizo zote sio namna ya kufanya meno kuwa masafi na kujikinga na wadudu wanaosababisha meno kuoza.

Amesema njia nzuri kwanza ni mswaki wenye brashi laini na dawa yenye floride na mtu anapopiga mswaki anatakiwa atumie dakika mbili baada ya hapo anatema povu na asiweke maji mdomoni.

“Unapopiga mswaki na kuweka maji mdomoni ukasukutua na kutema unakuwa umetoa dawa ambayo ilikuwa ni muhimu kwa meno kuoza.

Dk Kunji amebainisha kuwa mswaki unaotakiwa ni wenye brashi laini hivyo mtu akitumia mswaki wa mti ni mgumu na matokeo yake badala ya kusafisha meno ataumiza fizi.

“Wengi wamekuja na matatizo hayo fizi zinavidonda na pia meno yamekwaruzwa sana ile tabaka la juu inayolinda jino liko wazi na anapata maumivu hivyo sio njia sahihi na a kwa matumizi ya majivu yale hayana kiwango chochote cha floride kama mkaa na wengine wanatumia hadi sabuni na chumvi matokeo yake sio mazuri,”amesisitiza.

Kuhusu dawa za asili za meno amesema zinawekwa karafuu ambazo zinapunguza tu maumivu na haitibu hivyo maumivu yatapungua lakini madhara yake ni makubwa kwani jino litaendelea kuoza hadi kwenye kiini na jino kutengeneza jipu linalotoa usaha ambapo ule usaha ni hatari inaweza sababisha mtu kufa .

“Wengine wanatumia hadi mafuta ya betri ya gari wengine ya tranfoma wanaweka kwenye jino hizo njia ya matibabu sio nzuri unatuliza tu maumivu hujatibu tatizo.

Dk Kunji amesema kwasasa dawa ya jino sio kung’oa bali ni kufanya matibabu sahihi kulingana na tatizo lililopo, unaweza kuziba kawaida na kukata mzizi wa jino na hatua mwisho kabisa ni kung’oa.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *