Tusimamie malezi ya vijana- Dk.Mwinyi

ZANZIBAR: RAIS wa Zanzibar  na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Hussein Ali Mwinyi amewahimiza Wazazi na Walezi kuhakikisha wanasimamia malezi bora yenye maadili kwa watoto na  vijana.

Dk. Mwinyi  aliyasema hayo leo Julai 26 , 2024 alipojumuika na Waumini wa Dini ya Kiislam katika ibada ya sala ya Ijumaa  msikiti wa Sheikh Sharaan Meli nne Unguja.

Aidha Dk.Mwinyi ameleeza kuwa ni wajibu wa kila mmoja kuhakikisha anasimamia malezi ya watoto na vijana kutokana  kwa kuwa dunia imebadilika na sasa ni wakati wa utandawazi, hujifunza mengi kupitia mitandao ya kijamii.

Advertisement

Rais Dk.Mwinyi amewataka Wazazi na walezi kuhakikisha  wanawafundisha watoto na vijana elimu ya Dini ili kuwa taifa lenye raia wema na hofu ya Mungu.

SOMA: Samia asisitiza maadili bora kwa watoto