Tuzo taarifa za hesabu zaongeza uwajibikaji

DAR ES SALAAM: Naibu Waziri wa Fedha, Laurent Luswetula, amesema kuwa Tuzo za Ubora wa Uandaaji wa Taarifa za Hesabu kwa mwaka 2024 zimekuwa daraja muhimu katika kuimarisha uwajibikaji na uadilifu katika matumizi ya fedha za umma kwenye taasisi mbalimbali nchini.

Akizungumza katika hafla ya utoaji wa tuzo hizo jijini Dar es Salaam, Luswetula amesema zaidi ya taasisi 80 za umma na binafsi zimewasilisha taarifa zao za fedha kwa ajili ya ushindani huo, akitoa rai kwa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA) kuendelea kuzalisha wataalamu wenye weledi na maadili katika tasnia ya uhasibu na ukaguzi.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi ya NBAA, CPA Prof. Sylvia Temu, amesema tuzo hizo zimeendelea kutoa hamasa kwa taasisi kujikita katika kuandaa taarifa sahihi na zenye viwango vinavyokubalika kitaifa na kimataifa.

Miongoni mwa washindi wa tuzo hizo ni Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) na Wakala wa Usafirishaji Tanzania (TASAC), ambapo Kamishna Jenerali wa DCEA, Aretas Lyimo, amesema ushindi huo unaonesha matumizi sahihi ya fedha za Watanzania katika kutekeleza mipango ya maendeleo ya taifa.

Naye Mkurugenzi wa Fedha wa TASAC, CPA Pascal Karomba, amesema tuzo hizo ni kielelezo cha uwazi na nidhamu wanayoisimamia katika usimamizi wa rasilimali za umma.

Kwa upande wa serikali za mitaa, Mkoa wa Kigoma na Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma wameibuka washindi wa jumla, huku Mkuu wa Mkoa huo, Balozi Simoni Siro, akisema ushindi huo ni mwendelezo wa dhamira ya mkoa huo kutoa huduma bora na zenye tija kwa wananchi.

Habari Zifananazo

One Comment

  1. Google provides awesome remote work opportunities, allowing me to earn $2000-$3000 weekly with just 2-4 hours of daily work. It’s been a game-changer, offering flexibility and reliable income. If you’re seeking a genuine way to earn online, don’t miss this chance. Start today and transform your life!
    .
    More Details For Us →→ http://www.big.income9.com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button