Tuzo za Samia kalamu awards kutolewa Mei

DAR-ES-SALAAM : TUZO za Uandishi wa Habari za Maendeleo “Samia Kalamu Awards” zimepangwa kutolewa Mei mwaka huu.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA), kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) jijini Dar-es-salaam, mabadiliko haya yamefanyika kutokana na sababu za kiutendaji.
Hapo awali, hafla hiyo ilipangwa kufanyika tarehe 29 Aprili 2025 katika Ukumbi wa Mabele, Mabeyo Complex, jijini Dodoma.
Aidha waalikwa wote watatumiwa mwaliko mpya wenye maelezo kamili kuhusu eneo na ratiba ya tukio hilo.
SOMA: Wazalendo 79 kutunukiwa tuzo za habari za maendeleo
Mgeni Rasmi katika tukio hili anatarajiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan.



