Wazalendo 79 kutunukiwa tuzo za habari za maendeleo

DAR-ES-SALAAM: RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan, atatoa Tuzo za Waandishi wa Habari za Maendeleo 79, maarufu kama Samia Kalamu Awards, Aprili 29, mkoani Dodoma

Tuzo hizi zimeandaliwa kwa ushirikiano kati ya Chama cha Waandishi wa Habari Tanzania (TAMWA) na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA). SOMA: Ushiriki ‘Samia Kalamu Awards’ wasogezwa mbele

Mkurugenzi wa TAMWA, Dk. Rose Reuben, alitangaza washindi 79 kutoka maeneo mbalimbali nchini, ambao wamechaguliwa baada ya kazi zao kupitishwa na jopo la majaji na kupigiwa kura na wananchi.

Advertisement

Mhandisi Jan Kaaya, akimwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, alisema tuzo hizi zinatokana na mafunzo yaliyofanyika mwaka jana yanayolenga kukuza uandishi wa habari za maendeleo.

Tuzo zimegawanywa katika makundi matatu, ikiwa ni pamoja na Tuzo Maalumu za Kitaifa, Tuzo kwa Vyombo vya Habari, na Tuzo za Kisekta, zikiwa na lengo la kuhamasisha uandishi wa habari za maendeleo nchini.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *