TIMU ya taifa ya mpira wa wa miguu kwa Wanawake(Twiga Stars) inashuka dimbani leo kuikabili Tunisia katika mchezo wa Kombe la Wanawake la Tunisia 2024.
Mchezo huo utafanyika kwenye uwanja wa Terrain Ariana uliopo mji mkuu wa Tunisia, Tunis.
Mashindano hayo ya kimataifa yanayoanza leo hadi Julai 15 yakishirikisha timu tatu za taifa ambazo ni wenyeji Tunisia, Tanzania na Botswana yameandaliwa Shrikisho la Mpira wa Miguu Tunisia(FTF).
Twiga Stars itashuka tena uwanjani Julai 13 kuikabili Botswana.
Soma zaidi:http://Twiga Stars yatakata na kusonga mbele
Aidha michuano hiyo itatumika kama sehemu ya maandalizi ya awamu mwisho kwa ajili ya fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa Wanawake(WAFCON) Morocco2025.