Uchaguzi mitaa kutumia 4R za Rais za Samia

CHAMA Cha Mapunduzi(CCM) kimesema uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 27,2024 utaongozwa na 4R za Rais Samia Suluhu Hassan hasa kwa kuzingatia kuheshimiana na kuvumiliana.

Katibu wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi Taifa(CCM-NEC), Itikadi, Uenezi na Mafunzo ameeleza hayo leo Novemba 6,2024 akizungumza na viongozi na wanachama wa CCM Wilaya ya Ilala ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya mkoani Dar es salaam na Pwani.

“Tutofautiane tu kwa itikadi lakini tuna Tanzania moja, uchaguzi uiache Tanzania ikiwa moja ya amani na utulivu, CCM tunavyosema hivyo tunamaanisha kwa mambo yaliyofanywa na Dk Samia Suluhu Hassan kila mwana CCM akipewa nafasi ya kuongea ataongea mambo mengi yaliyofanywa,” amesema Makalla.

Advertisement

Amefafanua kuwa Chama hicho kinaahidi kufanya kampeni za kistaarabu na ameviomba vyama vingine vya siasa nchini kampeni zitakapoanza waende na R4 ,wajenge hoja.